Ban apokea ombi la Palestina kuwa mwanachama wa UM

23 Septemba 2011

Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas leo amewasilisha ombi rasmi kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon la kutaka Palestina kuwa taifa huru na mwanachama wa Umoja wa Mataifa.

Israel kwa upande wake haiungi mkono ombi hilo la Wapalestina kufikishwa kwenye Umoja wa mataifa bali inataka kuwe na majadiliano ya ana kwa ana baina ya pande hizo mbili.

Hii ni moja ya mada kubwa kwenye ajenda ya baraza hili kuu la 66 la Umoja wa Mataifa. Rais Abbas ambaye baada ya kukabidhi ombi hilo kwa Umoja wa Mataifa amehutubia baraza kuu na kusema baada ya miaka 63 ya mateso ni wakati sasa kwa watu wa Palestina kupata uhuru wao.

(SAUTI YA MAHMOD ABBAS)

Rais Abbas amemtaka Katibu Mkuu kuwasilisha ombi hilo kwenye baraza la usalama ambalo amelitaka kupiga kura kunga mkono uanachama kamili wa Palestina. Pia ameziomba serikali ambazo bado hazijalitambua taifa la Palestina kufanya hivyo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter