Baraza la usalama lataka kuboreshwa kwa mfumo wa UM

23 Septemba 2011

Baraza la Usalama hatimaye limeweka zingatio la juu kuhusiana na nafasi ya Umoja wa Mataifa kwenye kushughulikia mizozo na mikwamo ya kisiasa na wakati huo huo kuboresha shabaya ya utumiwaji wa diplomasia ya uzuiaji migogoro. Kakika kikao chake kilichowahusisha maafisa wa ngazi za juu na kuendeshwa na rais wake Michel Sleiman, baraza hilo limesema kuwa Umoja wa Mataifa unapaswa sasa kuchukua nafasi za usoni kabisa.

Kwa kauli pamoja maafisa hao wamekubaliana juu ya haja ya kuuboresha mfumo wa Umoja wa Mataifa ili uweze kuzikabili kirahisi changamoto za wakati huu zinazohusiana na mikwamo ya kisasa na migogoro ya hapa na pale. Ama limeweka zingatio kuhusiana na matumizi ya diplomasia ya uzuaji mizozo kujitokeza ikisema kuwa hiyo ndiyo shabaha muhimu ya kuleta utengamao

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter