Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zitaamua nani awe mjumbe asiye wa kudumu baraza la usalama:Ban

Nchi zitaamua nani awe mjumbe asiye wa kudumu baraza la usalama:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anasema kuwa ni wajibu wa wanachama wa umoja huo kuamua ni nchi zipi zinazoweza kuchukua nafasi za wanachama wasio wa kudumu kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na kukana madai kuwa anaunga mkono taifa fulani.

Hii ni baada ya madai kuwa Ban alikuwa akilipigia debe taifa la Hungary ili lipate kuwa mwanachama wa baraza la usalama wasio wa kudumu lenye wanachama kumi na tano.

Ili achaguliwe kuwa mwanachama asiye wa kudumu nchi mgombea lazima ipate uungwaji mkono wa thuluthi mbili ambapo pia uanachama huo unatolewa kwa kufuata masuala ya kijiografia. Wanachama watano wa kudumu katika baraza hilo ni pamoja na China, Ufaransa, Urusi, Uingereza na Marekani.