Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi nyingine 13 zasaini itifaki ya Nagoya

Nchi nyingine 13 zasaini itifaki ya Nagoya

Nchi nyingine 13 zimesaini itifaki ya Umoja wa Mataifa ambayo inaweka zingatio juu ya maridhiano ya pamoja kwenye utumiaji sawa na wa haki wa rasilimali zilizopo chini ya dunia. Mkataba huo unaojulikana kama Nagoya uliasisiwa mwaka uliopita nchini Japan ukitaka kuzihimiza nchi zote duniani kuwa na malengo ya pamoja hasa panapohusika na uzalishaji na utumiaji wa viumbe hai.

Umoja wa Mataifa hata hivyo amezihimiza nchi wanachama wake kuridhia mkataba huo ili uanze kufanya kazi mara moja. Jumla ya nchi 50 hadi sasa ndizo zilizosaini itifaki hiyo.