Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia inaungana na Walibya kujenga upya taifa lao:Obama

Dunia inaungana na Walibya kujenga upya taifa lao:Obama

Dunia iko pamoja na watu wa Libya wakati wakijenga upya mfumo wa kidemokrasia Huo ndio ujumbe uliotolewa na Rais Barack Obama wa Marekani wakati viongozi wa dunia waliokusanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa wakijadili suala la Libya leo Jumanne.

Rais Obama amesema bado kuna wakati mgumu mbele yao hasa ukizingatia kwamba wafuasi wa utawala wa Gaddafi uliopita wanaendelea kupigana.

(SAUTI YA RAIS BARACK OBAMA)