Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azindua kongamano la kupambana na ugaidi kwa wito wa ushirikiano

Ban azindua kongamano la kupambana na ugaidi kwa wito wa ushirikiano

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezindua kongamano la kimataifa la kupambana na ugaidi kwa wito wa kuimarisha shirikiano ili kukabili tatizo hilo ambalo linaathiri mataifa yote na kujenga dunia salama kwa wote.

Ban amesema kuwa kufanyika kongamano hili ametambua kuwa wote tuko katika vita pamoja. Kongamano hilo ni miongoni mwa mikutano ya ngazi ya juu ya wakuu wa nchi inayofanyika kwenye mkutano wa 66 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuanzia leo. Anasema kongamano hili litafungua ukurasa mpya katika ushirikiano wa kukabiliana na ugaidi, kwani mataifa yanatambua kwamba hayawezi kupinga vita peke yao, lakini kwa pamoja yanaweza kupata mbinu bora za kuushinda ugaidi.

Ban amekumbushia ari ya mataifa yote miaka mitano iliyopita walipoidhinisha mikakati ya kupambana na ugaidi na kendekea kupigia chepo mkataba wa kupambana na ukatili huo mkakati aliosema unatamba kwamba gaidi hawezi kumalizwa na masala ya usalama au kisheria pekee.

Amesema kumaliza ugaidi kunahitaji kujumuisha masuala ya kijamii, elimu, kiuchumi na kisiasa ambayo yatalenga chanzo cha ugaidi.

Ban pia ametangaza kwamba Umoja wa Mataifa umetia saini makubaliano na serikali ya Saudia wa kuanzisha kituo cha Umoja wa Mataifa cha kupambana na ugaidi au UNCCT katika taifa hilo.