Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yaahidi kuendelea kusaidia waathirika wa ukame Somalia

UNICEF yaahidi kuendelea kusaidia waathirika wa ukame Somalia

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF litaendelea kutoa msaada wa kibinadamu kwa Somalia mbayo inakabiliwa na njaa kwenye makambi na kwenye nchi za jirani ambako wakimbizi kutoka nchini humo wanapata hifadhi licha ya matarajio ya msimu mzuri wa mvua.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa kanda ya Afrika Mashariki na Kusini wa UNICEF Elhadj As Sy shirika hilo litaendelea kufuatilia kwa karibu hali inavyoendelea ili mafanikio ya leo yasiwe hatarini kwa kukosekana msaada.

Maelfu ya Wasomali wanakadiriwa kufa na wengine zaidi ya milioni 3.2 wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula kufuatia moja ya ukame mkubwa kabisa kwenye Pembe ya Afrika katika miongo sita, na kupanda kwa gharama ya chakula na vita kumezidisha hali kuwa mbaya zaidi.