Waliouawa mjini Abuja wakuumbukwa na UM
Umoja wa Mataifa umeandaa sherehe za makumbusho mjini Abuja nchini Nigeria kwa wafanyikazi wake waliouawa wakati makao yake yaliposhambuliwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga mnamo mwezi uliopita.
Kupitia kwa ujumbe uliowasilishwa kwa niaba yake na maratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Nigeria Daouda Touré katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa wito wa kutolewa kwa heshima kwa wale ambao wamejitolea kuhakikisha kuwa huduma za UM zinaendelea nchini humo. Wafanyikazi 11 wa Umoja wa Mataifa na watu wengine 12 waliuawa na wengine 116 wakajeruhiwa kwenye shambulizi hilo la agosti 26.