Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya amani duniani kwa wito wa kufanya sauti yako isikike:UM

Siku ya amani duniani kwa wito wa kufanya sauti yako isikike:UM

 

Umoja wa mataifa leo umeadhimisha siku ya kimataifa ya amani, ukiwaenzi wote ambao wanafanyaka kazi kwa kila hali kuwapa mstakhabali mzuri wengine na kutoa wito wa kuhakikisha sauti zao zinasikika ili kuimarisha amani na demokrasia.

Mwaka huu ni mwaka wa 30 tangu kuanza kuadhimishwa siku ya kimataifa ya amani ambayo kila mwaka hufanyika Septemba 21. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “amani na demokrasia, fanya sauti yako isikike”.

Akitoa ujumbe maalumu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni muhimu kwa haki za binadamu kutoa muongozo na njia za kutatua tofauti na kuwapa matumaini wasio nayo na kuwapa mamlaka watu. Lakini amesema demokrasia haitokei tu bali inahitaji kutafutwa na kutetewa, hasa kwa haki na huru, mazingira bora, kuwawezesha wanawake, utawala wa sheria na haki ya mtu kusema kuhusu hatima yake.

Siku hii imeambatana pia na matukio mbalimbali ikiwepo kugonga kengele ya amani, na ujumbe kutoka kwa mabalozi wema wa amani wa Umoja wa Mataifa akiwemo Jane Goodal.

(SAUTI YA JANE GOODAL)