Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matukio ya Afrika Kaskazini na mashariki ya kati yanadhihirisha kilio cha demokrasia:Ban

Matukio ya Afrika Kaskazini na mashariki ya kati yanadhihirisha kilio cha demokrasia:Ban

Matukio yaliyotia fora kuunga mkono mabadiliko ya kisiasa Afrika ya Kaskazini na Mashariki ya Kati yanadhihirisha kwamba demokrasia ni mfano wa utawala ambao watu wa utamaduni na mataifa tofauti wanalilia, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Akitoa ujumbe maalum wa siku ya kimataifa ya demokrasia hii leo Ban amesema dunia imeshuhudia ukweli wa msemo kwamba nchi haziwi imara kwa demokrasia bali zinakuwa imara kupitia demokrasia, hata hivyo ameongeza kuwa demokrasia hiyo haiwezi kuingizwa kutoka nje, watu wenyewe wataleta demokrasia.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “vijana na demokrasia” na amesema vijana zaidi ya kila mtu ndio walioleta ujumbe huo nyumbani. Amesema vijana ndio waliochagiza mabadiliko na sasa wanaishi kushuhudia matunda na changamoto za umuhimu wa mabadiliko waliochangia kuyaleta. Umoja wa Mataifa umekwa na jukumu kubwa la kuleta demokrasia duniani kwa kusaidia kufanyika kwa chaguzi huru na za haki, kuchagiza ushiriki wa jumuiya za kijamii na kushawishi mazungumzo pale pande mbili zinaposhindwa kuafikiana.