Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maamuzi ya leo yatakuwa na athari kubwa hapo kesho:Ban

Maamuzi ya leo yatakuwa na athari kubwa hapo kesho:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amewaeleza viongozi wa dunia wanaokutana kwenye mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York kuwa maamuzi ya leo yatakuwa na athari kubwa hapo kesho, hivyo ni lazima yafanywe kwa uangalifu na umakini mkubwa.

Ban amebainisha masuala matano muhimu ikiwemo bila rasilimali Umoja wa Mataifa hauwezi kutimiza majukumu yake akizungumzia, maendeleo, matatizo ya bajeti, suala la idadi ya watu kufikia bilioni 7, kuwawezesha wanawake na kuwekeza katika Umoja wa Mataifa. Kwanza Ban amefafanua kuhusu umuhimu wa maendeleo endelevu.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Amesema pia mkakati wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Rio+20 lazima ufanikiwe na hatua ipigwe kukabiliana na mabadiliko hayo. Ameongeza kuwa suala la nishati ni muhimu na ni lazima kuwekeza katika sekta hiyo kwa manufaa ya watu. Lakini pili amegusia suala la bajeti akisema bajeti ya masuala ya kulinda amani itafikia bilioni dola bilioni 8 na kupunguza bajeti amesisitiza itakuwa bora kuzia migogoro kabla haijatokea ambapo itagharimu sana kupeleka vikosi vya kulinda amani.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Tatu Ban amesisitiza umuhimu wa kujenga dunia salama, kwani huo ndio wajibu wa Umoja wa Mataifa, amesema mwaka huu kumekuwa na changamoto nyingi akitaja matatizo ya Ivory Coast, Afghanistan na Iraq ambako anasema dunia imesimama pamoja kutafuta suluhu ya kisiasa ya matatizo hayo na juhudi zinaendelea kwa nchi kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Somalia na Sierra Leone. Hata hivyo katika suala lake la nne amezungumzia fursa kubwa ya kuunga mkono mataifa katika kuleta mabadiliko.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Fursa kubwa ya nne ni kusaidia mataifa katika kipindi cha mpito, matukio ya mwaka huu Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati yametutia motisha,Tusaidie kufanya machipuko ya ulimwengu wa kiarabu kwa msimu wa matumaini ya kweli kwa wote, na Umoja wa Mataifa lazima utafute njia iliyo bora kutimiza matumaini hayo. Hatimaye amegusia sala la kuwawewezesha wanawake na vijana.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ban aliyekuwa akizungumza kabla ya kuanza mjadala wa baraza kuu hii leo amemalizia kwa kusema lazima dunia iende sambamba na mabadiliko, katika wakati huu wa matatizo ya fedha dunia lazima ijitahidi kufanya mambo mengi kwa fedha kidogo na kuwekeza na kuzitumia vyema fedha za walipa kodi.