Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza kuu la UM laadimisha miaka kumi ya mashambulio ya kigaidi ya Septemba 11

Baraza kuu la UM laadimisha miaka kumi ya mashambulio ya kigaidi ya Septemba 11

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa leo limekutana katika hafla maalumu ya kumbukumbu ya miaka 10 tangu kufanyika mashambulio ya kigaidi yaliyoitikisha dunia hapa Marekani Septemba 11 mwaka 2001. Katika mashambulio hayo maelfu ya watu walipoteza maisha, mustakhabali wa maelfu kusambaratishwa na mamilioni kusalia na majeraha ambayo ni vigumu kusahau.

Akizungumza katika hafla hiyo Rais wa baraza kuu ambaye anamaliza muda wake Josef Deiss amesema hii ni kumbukumbu ambayo watu wangetumai kutoiadhimisha kutokana na historia ya machungu na majeraha yaliyosababishwa na shambulio hilo. Amesema ugaidi ni vitendo vinapingwa vikali na Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa na nguvu za pamoja zinahitajika.

(SAUTI YA JOSEF DEISS)

Katika hafla hiyo Naibu Katibu Mkuu Asha Rose Migiro amesema ili kuwaenzi vyema waliopoteza maisha na kuathirika katika shambulio hilo lazima tuungane kupambana na ugaidi.

(SAUTI YA ASHA ROSE MIGIRO)

Amesema licha ya hatua zinazoendelea kuchukuliwa kukabiliana na ugaidi, watu bado wanatekeleza vitendo hivyo akitoa mfano wa mashambulizi ya Agosti 26 kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa Abija Nigeria na amezitaka nchi wanachama kuwa msitari wa mbele katika vita dhidi ya ugaidi.