Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vifo vya watoto wachanga vyapungua lakini bara la Afrika lasalia nyuma

Vifo vya watoto wachanga vyapungua lakini bara la Afrika lasalia nyuma

Utafiti Mpya kutoka kwenye shiririka la afya duniani WHO pamoja na washirika wake unaonyesha kuwa idadi ya watoto wanaokufa baada ya mara baada ya kuzaliwa imeungua kote duniani lakini hata hivyo maendeleo yanajikokota huku bara la Afrika likiachwa nyuma. Vifo vya watoto wanaozalia vilipungua kutoka watoto milioni 4.6 mwaka 1990 hadi watoto milioni 3.3 mwaka 2009. Kulingana na utafiti huo uliongozwa na watafiti kutoka WHO uliohukua miaka 20 na uliondeshshwa kwenye nchi 193 wanachama wa WHO ulipata kuwa vifo vinavyotokea wiki nne baada ya mtoto kuzaliwa vinachukua asilimia 41 ya vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano. Karibu asilimia 99 ya vifo vya watoto wanaozaliwa hutokea kenye ulimwengu unaondelea huku zaidi ya nusu vikitokea nchini India, Nigeria, Pakistan, China na Jamhuri ya Kidemkrasia ya kongo..