Mkutano wa kujadilia fursa za afya wafanyika Geneva
Kongamano la kujadilia njia bora zitazowawezesha watumiaji wa huduma za afya namna wanavyofikia kirahisi na huduma hizo, umeanza leo huko Geneva, kwa mkurugenzi wa shirika la afya duniani WHO kutoa wito kwa mataifa kubadilisha mwenendo wa kushughulia matatizo ya sekta ya afya.
Bi Margaret Chan ameuambia mkutano huo wa siku moja kuwa bado kuna msururu mrefu wa mahitaji ambayo nchi husika zinawajiba kujifunga kibwebwe ili kutatua changamoto hizo.
Amesema hata hivyo wimbi jipya la mabadiliko kwenye sekta ya afya kumezilazimu nchi mbalimbali kubadilisha mkondo wa uendeshaji mambo hatua ambayo amesema kuwa bado haijajibu ipasavyo mahitajio muhimu.
Amedokezea pia kuhusu kuendelea kushamiri kwa magonjwa yasiyoambukiza kama shinikizo la damu, kansa kuwa sasa yanawaelemea zaidi wato maskini ambao hawana uwezo wa kuyagharimia.