Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya kimataifa ya Uhisani UM wasisitiza umuhimu wa watu kuwasaidia watu

Siku ya kimataifa ya Uhisani UM wasisitiza umuhimu wa watu kuwasaidia watu

Leo Umoja wa Mataifa unaadhimisha mwaka wa tatu tangu kuanzishwa siku ya kimataifa ya wahisani, huku hafla zikifanyika duniani kote. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “watu kusaidia watu”, siku hii inaadhimishwa wakati mashirika ya misaada yakiongeza juhudi kuwasaidia mamilioni ya watu walio katika hali mbaya kwenye pembe ya Afrika na kwingineko, na wakati ambapo wafadhili na jamii mbalimbali zikiendelea kujitolea.

Umoja wa mataifa unasema hii ni fursa mhimu ya watu kutafakari kuhusu kazi za kokoa maisha zinazofanywa na wafanyakazi wa misaada, wengi katika maeneo ya hatari, kwenye jamii zao au mbali sana na nyumbani kwao.

Katika hafla maalumu kwenye makao maku ya Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu Ban Ki-moon, mku wa OCHA Valarie Amos na mkuu wa UNICEF Anthony Lake wamezungumzia kazi zinazofanywa na wahisani. Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Wakiwakumbuka wafanyakazi wenzao waliopoteza maisha wakiwasaidia wengine Valarie Amos amesema siku hii ni kuhusu hiba au urithi waliouacha, kuwaenzi na kuendeleza walichokuwa wakifanya, na kujitahidi kwa kila njia kusaidia wengine kwa mamilioni wanaotaabika pembe ya Afrika.

Naye mkurugenzi mku wa UNICEF Anthony Lake akizungumzia mchango wa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa amesema ni ya kwaenzi wafanyakazi wa kitaifa na kimataifa wa ambao wamejitolea sio tu kusaidia watoto katika nchi zao bali pia mustakabali wa nchi hizo, akiwakumbuka pia wafanyakazi 23 wa Umoja wa Mataifa waliofariki dunia kwenye shambulio la bomu miaka minane iliyopita mjini Baghdad Iraq.

Na kwa kuwaenzi wahisani wote wimbo maalumu umetolewa leo ukishirikisha wanamziki mbalimbali duniani akiwemo Ziggy Marley na Beyonce, wimbo unaitwa "If I could change” Kama ningeweza kubadili dunia.

(WIMBO IF I COULD CHANGE)

Watu kutoka sehemu mbalimbali siku hii wamekuwa wakitoa ujumbe maalumu, wasikilize hawa kutoka Afrika ya Mashariki.

(MAONI AFRIKA MASHARIKI)