Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wengi waishio Libya hawana huduma muhimu-IOM

Wahamiaji wengi waishio Libya hawana huduma muhimu-IOM

Kundi kubwa la wahamiaji wanaishi huko Libya wanaendelea kusota bila huduma muhimu ikiwemo maji, nishati ya umeme na usalama wa hali za afya.Kulingana na tathmini iliyofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM, wahamiaji hao ambao wapo kwenye kambi iliyoko kwenye mji wa Al-Kufrah ulioko Kusin mashariki mwa Libya, wapo kwenye wakati mgumu.

Kambi hiyo ambayo ilianzishwa miaka kadhaa ya nyuma ni kitovu muhimu cha kuelekea katika eneo la Benghazi na barani Ulaya. Hadi sasa inachukua jumla ya wahamiaji 15,000 . Shirika hilo la Umoja wa Mataifa katika taarifa yake limesema kuwa limebaini kuwepo kwa wahamiaji kati ya 3,000 hadi 4,000 ambao wanakabiliwa na hali mbaya kutokana kuendelea kuishi bila huduma muhimu.