Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazindua muongozo kwenye mtandao kusaidia kukabili mifumo ya utapia mlo

UM wazindua muongozo kwenye mtandao kusaidia kukabili mifumo ya utapia mlo

Serikali na wafanyakazi wa afya sasa wanaweza kupata taarifa za mpango mya ulioanzishwa na shirika la afya duniani WHO kwa njia ya mtandao, wenye lengo la kutoa mwongozo mpya wa kisayansi kudhibiti vitisho vya afya vinavyosababishwa na utapia mlo.

Mpango huo mpya wa WHO uitwao e-mkataba ambao ni ushahidi kuwa hatua za lishe (eLENA) na taarifa maalum za kupambana na mifumo mitatu ya utapia mlo, ikiwemo uzito mdogo, upungufu wa madini na vitamin mwilini na tatizo la uzito wa kupindukia.

WHO inakadiria kwamba watoto milioni 3.9 wanakufa kila mwaka kutokana na uzito mdogo wakati watoto zaidi ya milioni 40 wenye umri wa chini ya miaka mitano wana matatizo ya kuwa na uzito wa kupindukia. Dr Francesco Branca ni mkurugenzi wa lishe katika idara ya afya na maendeleo ya WHO.

(SAUTI YA FRANCESCO BRANCA)