Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shughuli za kusafirishwa kwa misaada kwenda nchini Somalia kung’oa nanga

Shughuli za kusafirishwa kwa misaada kwenda nchini Somalia kung’oa nanga

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema kuwa shughuli za kusafirishwa kwa misaada kwenda nchini Somalia huenda zikang’oa naga hii leo. Msemaji wa WFP Emilia Casella amesema kuwa ndege zitasafirisha chakula kwa watoto wanaosumbuliwa na utapia mlo na misaaada mingine.

Nalo shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa  (UNICEF)  kwa ushirikino na wizara ya afya nchini Kenya pamoja na shirika la afya duniani WHO wamezindua kampeni ya kutoa chanjo ambayo itawalenga zaidi ya watoto 200,000 wanaoishi kwenye maeneo yanayokumbwa na ukame karibu na kambi ya Daadab. Msemaji wa UNICEF Marixie Mercado anasema kuwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio na tembe za kuua minyoo vimejumuishwa kwenye kampeni hiyo.