Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waainisha changamoto zinazoikabili Sudan Kusin

UM waainisha changamoto zinazoikabili Sudan Kusin

Umoja wa Mataifa umezianisha changamoto zinazolikabili taifa jipya la Sudan Kusin na kuhaidi kuweka msaada wa hali na mali ili kulipiga jeki taifa hilo lilipata uhuru wake baada ya kujitenga na Sudan. Kulingana na Naibu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na usamaria mwema, Lise Grande,Sudan Kusin inviashirio vingi ambavyo vinakwaza kupatikana kwa maendeleo.

Akizungumza kwenye mkutano wa kimataifa huko Geneva, Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amehaidi kuendelea kuliunga mkono taifa hilo na kwa kuanzia itaweka zingatio katika maeneo muhimu ambayo ni maeneo yaa kiutu, ujenzi wa jamii imara na mifumo ya sheria,kuandaa mazingira ya kukuza mifumo ya kiutendaji.Taifa hilo la Sudan Kusin lenye idadi ya watu wanaofikia milioni 9, linakabiliwa na changamoto ya umaskini ambao wengi wao ni vijana na wakazi wa vijijini.