Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya kwanza ya kimataifa ya mahakama ya kimataifa ya ICC yaadhimishwa

Siku ya kwanza ya kimataifa ya mahakama ya kimataifa ya ICC yaadhimishwa

Miaka 13 baada ya kubuniwa kwa mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC, sasa mahakama hiyo imesherekea siku yake ya kwanza ya kimataifa ambayo ni tarehe 17 mwezi Julai. Mahakama hiyo ilibuniwa kwa lengo la kupambana na ukwepaji wa sheria na vitendo vya uhalifu chini ya makubalino ya Roma na ilianza kazi yake mwaka 2002 mjini Hague. Sang-Hyun Song ni rais kwenye mahakama ya ICC.