Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani vikali shambulizi la kigaidi India

UM walaani vikali shambulizi la kigaidi India

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ,Baraza la Usalama, wote kwa pamoja wamelaani vikali tukio la mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa kwenye maeneo mbalimbali ya mji wa Mumbai na kueleza kuwa vitendo kama hivyo havikubaliki.

Kwenye mashambulizi hayo, zaidi ya watu 20 waliuwawa na wengine 100 walijeruhiwa.Ban na Baraza la Usalama wameelezea masikitiko yao kwa waathirika wa tukio hilo na kwa serikali ya India. Baraza la Usalama ambalo limeelezea tukio hilo kama ukatili uliopindukia limesisitiza haja ya kukabiliana na vitendo vya ugaidi.