Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa kuendelea kushiriki kwenye mazungumzo ya Cypriot

Umoja wa Mataifa kuendelea kushiriki kwenye mazungumzo ya Cypriot

Viongozi wa jamii za Cypriot za nchini Uturuki na ugiriki wamekubali kuendelea kushiriki kwa Umoja wa Mataifa kwenye mazungumzo ya kuiunganisha Cyprus. Kisiwa hicho kimegawanyika tangu mwa 1974 wakati Uturuki iliwatuma wanajeshi wake kufuatia mapinduzi yaliyoandeshwa na wanajeshi nchini Uturuki.

Mapema leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alifanya mkutano wake wa tatu na viongozi wa Cypriot, Dimitris Christofias na Dervis Eroglu. Farhan Haq na naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa

(SAUTI YA FARHAN HAQ)

Ban amesema kuwa anaamini kuwa wakati watakutana naye mwezi Oktoba viongozi hao wataeleza maendeleo ya makubalino kwenye masuala muhimu.