Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa Um kuviunganisha visiwa vya Cyprus waleta matumaini

Mpango wa Um kuviunganisha visiwa vya Cyprus waleta matumaini

Viongozi wa Cyprus ya Ugiriki na Uturuki wameanza kuonyesha ishara ya kufikia makubaliano juu ya mzozo wao wa muda mrefu ambao pande zote mbili zimekuwa zikileta utata juu ya wazo la kuungana.

Hatua hiyo inakuja wakati viongozi wa pande zote mbili wakijiandaa kukutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon baadaye mwezi huu huko Geneva. Umoja wa Mataifa umekuwa ukiendesha juhudi zake za kidiplomasia kwa shabaya ya kutaka kuziunganisha pande zote mbili zilizoko kwenye kisiwa cha Mediterranean.

Viongozi hao Dimitris Christofias, na Dervis Eroglu watakuwa tena na mazungumzo ya pamoja wiki ijayo kulainisha tofauti zao kabla ya kusafiri hadi Geneva kwa mkutano na Ban Ki-moon.