Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bei ya nafaka yapungua huku bei ya mahindi ikisalia kuwa juu

Bei ya nafaka yapungua huku bei ya mahindi ikisalia kuwa juu

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO limesema kuwa bei za nafaka zilipungua kidogo kwenye masoko ya kimataifa mwezi Juni mwaka huu lakini hata hivyo bei hizo ziko asilimia 71 zaidi na mwaka uliopita . Hata hivyo bei ya mahindi inasalia kuwa ya juu kutokana na mazao ya chini ya mwaka 2010 na mvua nyingi nchini Marekani.

Kwa ujumla makadirio ya bei ya chakula ya FAO yaliongezeka kwa asilimia moja mwezi uliopita huku makadirio ya bei ya sukari yakiongezeka kwa asilimia 14 kati ya mwezi wa Mei na Juni wakati ambapo uzalishaji wa sukari nchini Brazil ambaye ndiye mzalishaji mkubwa wa sukari ukitabiriwa kushuka .Wakati huohuo matumizi ya nafaka mwaka 2011 n1 2012 yanatabiriwa kuongezeka kwa asilimia 1.4 hadi tani milioni 2,307 ikiwa ni tani milioni tano zaidi ya zilizotabiriwa.