Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UM kuzuru Namibia kutilia uzito masuala ya maji safi na salama

Mjumbe wa UM kuzuru Namibia kutilia uzito masuala ya maji safi na salama

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anajiandaa kufanya ziara rasmi nchini Namibia ambako anatazamiwa kujishughulisha na masuala ya maji pamoja na mifumo ya usafi.Catarina de Albuquerque anatazamiwa kuanza ziara yake July 4-11 ambako atakagua hali jumla ya upatikanaji wa maji hasa zaidi maeneo yale ambayo watu wake wako kwenye hali ya shida kufikiwa na huduma hiyo.

Mwishoni mwa ziara yake anatazamiwa kutoa mapendekezo ambayo yatazingatia hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kubadili hali ya mambo.Akiwa kama mtaalamu wa masuala ya haki za binadamu,Bi Catarina amesema kuwa ziara yake hiyo inachukua shabaya ya kuangalia makundi yaliyo pembezoni kama kweli yanafikiwa na huduma muhimu ya maji safi na salama kwani hilo ni moja ya mambo makuu yanayoanishwa kwenye mikataba ya haki za binadamu.