Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aridhishwa na duru ya kwanza ya uchaguzi Benin

Ban aridhishwa na duru ya kwanza ya uchaguzi Benin

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepongeza mafanikio ya awamu ya kwanza ya uchaguzi wa urais iliyoendeshwa kwa njia ya amani nchini Benin akisema kuwa taifa hilo la Afrika magharibi limekuwa mfano bora kwa kupanga uchaguzi bila ya kuripotiwa visa vyovyote.

Awamu hiyo ya kwanza ya uchaguzi ambayo tayari imehairishwa mara mbili iliandaliwa hapo jana huku vyombo vya habari vikiripoti kuwa huenda rais Boni Yayi na mgombea wa upinzani Adrien Houngbedji wakaingia kwenye awamu ya pili ya uchaguzi huo.

Kupitia kwa msemaji wake Ban alipongeza wagombea wote wawili na pia kuwataka kukubali matokeo ya mwisho na kusuluhisha kwa njia ya amani tofauti zozote ambazo zinaweza kuibuka kufuatia uchaguzi huo.