Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanamuziki nyota wa Mali watoa wimbo kupinga njaa

Wanamuziki nyota wa Mali watoa wimbo kupinga njaa

Wanamuziki mashuhuri duniani kutoka Mali mke na mume,  Amadou na Mariam ni miongoni mwa watu mashuhuri kujiunga katika harakati za kupambana na njaa duniani katika siku za hivi majuzi kama mabalozi wema wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP kwenye jumuiya ya ulaya.

Kwenye wimbo wao mpya wanamuziki hao wanazungumzia waliyoyashuhudia nchini Haiti ambayo alitembelea miradi ya WFP inayofadhiliwa na jumuiya ya ulaya.

Wimbo huo unaombatana na kanda ya video umezinduliwa hii leo Jumatatu 27 mjini Roma Italia.

Wakiwa nchini Haiti wanamuziki hao walikuwa na fursa ya kukutana na wanawake wajawazito pamoja na wanaolea watoto wadogo pamoja na watoto wao kwenye kambi ya Aviation ambapo watu 25,000 ambao makaazi yao yaliharibiwa wakati kulipotokea tetemeo la ardhi mwaka 2010 bado wameweka kambi.