Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti kuhusu hali ya kijamii duniani 2011 imetolewa:UN-DESA

Ripoti kuhusu hali ya kijamii duniani 2011 imetolewa:UN-DESA

Ripoti kuhusu hali ya kijamii dniani kwa mwaka huu wa 2011 iitwayo The Global Social Crisis iliyotolewa leo na idara ya Umoja wa Mataifa ya uchumi na masuala ya kijamii UN-DESA imebaini kwamba serikali nyingi hazitilii maanani sana athari za kijamii zitokanazo na mdororo wa kiuchumi duniani.

Ripoti inasema sera za kiuchumi zinachukuliwa kama ni za kipekee na kutengwa na athari zake kwa jamii, jambo ambalo mara nyingi linaleta matatizo kwa lishe ya watu, afya na elimu mambo ambayo yasiposhughulikiwa kwa muda mrefu yana madhara makubwa kwa ukuaji wa uchumi.

Kwa mujibu wa naibu katibu mkuu wa wa maendeleo ya kiuchumi wa UN-DESA Jomo Kwame Sundaram matatizo ya kiuchumi yanakumbusha kwamba ni muhimu kwa watu kuwa na afya bora, kuelimika, kuwa na nyumba zinazofaa na kulishwa ipasavyo ili waweze kuzalisha na kuchangia ipasavyo katika jamii. Lakini amesema serikali nyingi hazijatilia maanani athari za mgogoro wa kiuchumi kwa jamii zao.

(SAUTI YA JOMO KWAME SUNDARAM)

Ripoti hiyo imeongeza kuwa ongezeko la umasikini, njaa na kukosa ajira kutokana na matatizo ya kiuchumi litaendelea kuathiri mamilioni ya watu duniani kwa miaka mingi ijayo.