Biashara ina jukumu kubwa sana katika kukuza uchumi na kumaliza umasikini:UNCTAD

15 Juni 2011

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na biashara na maendeleo UNCTAD limesema biashara ina jukumu kubwa sana katika kuchangia ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini kwenye nchi zinazoendelea.

UNCTAD inasema biashara inasaidia kuzichipuza tena nchi baada ya mdororo wa uchumi na kupandisha viwango vya maisha ya mabilioni ya watu masikini duniani . Hayo yamesisitizwa katika mkutano wa juma zima unaofanyika mjini Geneva kuhusu mchango wa biashara kwenye uchumi. Mwenyekiti wa tume ya biashara na maendeleo Tom Mboya Okeyo kutoka Kenya amesema ujumbe katika mkutano huo wa tatu wa kila mwaka ni kwamba wanawake, watoto na vijana wanaamka kila siku wakihitaji chakula na ili wapate chakula wanahitaji ajira, na ajira hizo zitatoka wapi kama hakuna usawa katika biashara? George Njogopa anaarifu.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter