Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka wanawake kushirikishwa zaidi kwenye siasa

UM wataka wanawake kushirikishwa zaidi kwenye siasa

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa lililotwikwa jukumu la kuhakikisha kuwepo kwa usawa wa kijinsia amesema kuwa kuwainua wanawake kiuchumi , kuwashirika kwenye siasa na pia katika kutafuta amani baada ya mizozo ndiyo malengo ya shirika hilo.

Akihutubia mkutano wa waandishi wa habari mjini Geneva Michelle Bachelet amesema kuwa ofisi yake itashirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika wake katika masuala yakiwemo elimu kwa wanawake na wasichana pamoja na afya ya uzazi. Akizungumzia suala la dhuluna za kingono dhidi ya wanawake Bachelet amesema kuwa kuzuia ndiyo njia kuu ya kukabiliana na suala hilo. Amesema kuwa kuzuia ni pamoja kutoa hamasisho na kuwapa mafundisho watoto wasichana na wavulana kuhusu kuondoa ubaguzi ya kijinsia katika jamii.