Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya walinda amani 14,00 watafuta ushauri na kupimwa HIV

Zaidi ya walinda amani 14,00 watafuta ushauri na kupimwa HIV

Idadi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaotafuta ushauri nasaha na kupimwa kwa hiyari virusi vya HIV imeongezeka kutoka 2000 hadi zaidi ya 14,000 kwa kipindi cha miaka mitano.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon ametoa takwimu hizo kwenye baraza la usalama wakati likijadili athari za HIV na ukimwi katika suala la amani ya kimataifa na usalama.

Ban amesema kwamba ni taratibu kwa Umoja wa Mataifa kutoa mafunzo ya HIV kwa wafanyakazi wake kabla hawajatumwa kwenda kulinda amani.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Baraza la usalama linalokutana kujadili masuala ya HIV na ukimwi limehudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu wa serikali wakiwemo baadhi ya maraisi kutoka nchi wanachama walio na viti kwenye baraza hilo.