Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe maalum wa UM kuhusu ghasia dhidi ya watoto atoa wito wa kulindwa kwa watoto nchini Syria

Mjumbe maalum wa UM kuhusu ghasia dhidi ya watoto atoa wito wa kulindwa kwa watoto nchini Syria

Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon kuhusu ghasia dhidi ya watoto Marta Santos Pais ameelezea wasiwasi wake kuhusinia na ghasia wanazopitia  watoto kwenye mzozo unaoendelea nchini Syria. Mjumbe huyo anaishauri serikali ya Syria  kuwahakikishia usalama watoto wote kulingana na sheria za haki za watoto kwenye makubalino ya Marrakesh yaliyotiwa sahili Disemba iliyopita na mkutano wa kiarabu kuhusu haki ya mtoto.