Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jessica aliyezunguka dunia awa balozi mwema wa WFP

Jessica aliyezunguka dunia awa balozi mwema wa WFP

Raia wa Australia Jessica Watson ambaye ni baharia wa mwaka, amechaguliwa  kuwa mwakilishi wa vijana katika shirika la umoja wa mataifa linalohusika na mpango wa chakula.

Jessica mwenye umri wa miaka 18, May mwaka jana aliweka rekodi ya aina yake pale alipofahuru kuwa kijana mdogo zaidi duniani kusafiri majini kwa kuzunguka maeneo mbalimbali ya dunia.

Kwa kuwa mwakilishi wa  WFP anatazamiwa kutumia nafasi yake hiyo kuweka msukumo utakohamasisha ulimwengu juu ya umuhimu wa kiufadhilia miradi ya chakula ili kuzizaidia shule kadhaa.

Kila mwaka WFP hutoa msaada wa chakula kwa wanafunzi wanaofikia milioni 22 katika nchi 60.