Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon yuko ziarani Nigeria

Ban Ki-moon yuko ziarani Nigeria

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon yuko ziarani nchini Nigeria ambapo tayari amefanya mkutano na waziri wa mambo ya kigeni nchini humo Henry Odein Ajumogobia. Wawili hao walizungumzia uhusianao kati ya Nigeia na Umoja wa Mataifa. Pia walizungumzia umuhimu wa muungano wa Afrika katika kusuluhisha mzozo nchini Libya na pia kujitolea kwa Nigeria katika kuunga mkono miradi ya kiafya kwa akina mama na watoto kama moja ya njia ya kutimizwa mwa maelengo ya kifya ya maendeleo ya milenia.

Ban pia anatarajiwa kuhudhuria mkutano na kamati ya rais kuhusu malengo ya milenia kabla ya kutembelea kituoa cha afya ya Dutse Makarasa na kuhutubia mabalozi mjini Abuja.