Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

GEF yatoa dola zaidi ya milioni 2 kwa UN-Habitat na UNEP kusaidia nishati Afrika Mashariki

GEF yatoa dola zaidi ya milioni 2 kwa UN-Habitat na UNEP kusaidia nishati Afrika Mashariki

Nishati inayotumika katika majengo ni asilimia kubwa ya matumizi yote ya nishati katika nchi za Afrika ya Mashariki. Zaidi ya asilimia 40 ya umeme unalozalishwa katika nchi zinazoendelea unatumika katika majengo pekee maeneo ya mijini ikiwa ni zaidi ya nishati inayotumika na sekta ya usafiri na viwanda.

Sasa mradi maalumu ulioanzishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT, shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP kwa ushirikiano na serikli za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi una lengo la kusaidia matumizi bora ya nishati.

Mradi huo unataka kuwe na hatua maalumu za sera za majengo na shughuli za ujenzi Afrika Mashariki ili kuweza kuweza kuhifadhi nishati na kupunguza gesi za viwandani. Mashirika hayo yanasema mahitaji ya umeme yanaongezeka haraka katika nchi hizo kuliko kiwango cha uzalishaji hali iliyosababisha kupanda kwa gharama za umeme na hasa katika matumizi ya majumbani. Mradi huo utachukua miaka minne kuanzia mwaka huu hadi 2015 na utaendeshwa na UN-HABITAT kwa ushirikiano na wizara za nyumba za Afrika ya Mashariki. Na umepewa msaada wa dola milioni 2,853,000 na kitengo cha kimataifa cha mazingira GEF.