Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhusiano wa kiuchumi Afrika utaliinua bara hilo:UM

Uhusiano wa kiuchumi Afrika utaliinua bara hilo:UM

Uhusiano wa masuala ya uchumi baina ya nchi za bara la Afrika na kuwepo kwa sera ambazo zinayajali maslahi ya watu maskini vinaweza kuchangia kuinua maisha ya watu wengi hata hadi asilimia 10 kwa muda wa miaka kumi inayokuja.

Hii ni kulingana na ripoti kutoka kwa shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa iliyotolewa kwenye mkutano wa nchi maskini zaidi duniani unaoendela mjini Istanbul nchini Uturuki ripori inayotoa wito wa kwepo uwekezaji katika sekta muhimu kama vile barabara , nishati na kurahisisha kupatikana kwa huduma za umma.

Ripoti hiyo pia inasema kuwa mafanikio ya kiuchumi yatakuwepo tu ikiwa kutakuwa na uungwaji mkono wa kisiasa na kujitolea kwa viongozi kutoka serikali za kiafrika.