Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tani zaidi ya bilioni moja za chakula hupotea kila mwaka :FAO

Tani zaidi ya bilioni moja za chakula hupotea kila mwaka :FAO

Utafiti uliofanywa na shirika la chakula na kilimo FAO umebaini kwamba theluthi moja ya chakula kinachozalishwa kila mwaka kwa ajili ya matumizi ya binadamu duniani, sawa na tani takribani bilioni 1.3 kinapotea au kuharibika.

Utafiti huo ulioitwa “upotevu na utupwaji wa chakula duniani, umeandaliwa na FAO na kufanywa na taasisi ya chakula na teknolojia ya bailojia ya Sweeden kwa madhununi ya kuokoa chakula.

Matokeo ya utafiti huo yatawasilishwa rasmi kwenye kongamano la kimataifa kuhusu sekta ya kufunga vyakula litaklofanyika mjini Dusseldorlf Ujerumani Mai 16 hadi 17. Utafiti huo pia umebaini kwamba nchi zote zilizoendelea na zinazoendelea zinashabihiana kwa upotevu huo wa chakula. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)