Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Yemen na UNHCR wajadili hali ya wakimbizi wa Somalia

Yemen na UNHCR wajadili hali ya wakimbizi wa Somalia

Kamishina wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Yemen Claire Bourgeois na gavana wa jimbo la Lahj Yemen bwana Ahmed al-Majid mwishoni mwa wiki wamejadili hali ya wakimbizi wa Somalia walioko kwenye kambi ya Kharaz.

Katika mkutano wao Bi Bourgeois na Al-Majid wamezungumzia mambo watakayoshirikiana baina ya uongozi wa Yemen na ofisi ya UNHCR Aden, masuala hayo ni pamoja na kuanzishwa miradi kambini hapo na kuhakikisha masuala ya huduma za maji na usafi. George Njogopa anaarifu

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)