Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakuu wa masuala ya utawala wa sheria wa UM wahitimisha mkutano New York

Wakuu wa masuala ya utawala wa sheria wa UM wahitimisha mkutano New York

Wakuu wa masuala ya utawala wa sheria wa vitengo mbalimbali vya Umoja wa mataifa wamekamilisha mkutano wao wa juma zima uliokuwa ukifanyika hapa New Yory kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Wakuu hao pamoja na mambo mengine wamekuwa wakijadili changamoto na msaada wa kisheria katika shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa kwenye sehemu mbalimbali duniani.

Mkutano huo ulioandaliwa na idara ya operesheni za kulinda amani ya Umoja wa Mataifa na uliwaleta pamoja maafisa wanaohusika na masuala ya magereza, washauri wa kisheria, wakuu wa polisi wa Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa sheria wakichanganua mada ya utawala wa sheria katika shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa.

Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ni Jairus Gilbert Omondi  ambaye ni  afisa wa kurekebisha tabia katika magereza kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika wa kulinda amani Darfur UNAMID, nimejadili naye masuala mbalimbali na kwanza anafafanua mada na umuhimu wake.

(MAHOJIANO NA JAIRUS GILBERT OMONDI )