Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miradi 65 ya kukuza demokrasia kufadhiliwa:UM

Miradi 65 ya kukuza demokrasia kufadhiliwa:UM

Fuko la umoja wa mataifa linalohusika na ufadhili wa miradi ya demokrasia UNDEF limeorodhesha miradi ipatayo 65, ikiwemo 10 inayotoka katika nchi za kirabu ambayo inatazamiwa kupatiwa fedha kwa ajili ya kuendeleza shughuli za ukuzaji demokrasia.

Miradi hiyo ambayo imevuka hatua ya awali ni pamoja itayoendeshwa barani Afrika ambayo inachukua asilimia 34,wakati asilimia 23 ni kutoka barani Asia na asilimia 15 kutoka nchi za kiarabu ikiwemo Tunisia, Msri, Algeria na Morocco.

Kiasi cha fedha dola za kimarekani milioni 14 tayari kimetengwa na kinasubiri kuidhinishwa rasmi ka Katibu Mkuu Ban Ki-moon. Fuko hilo la umoja wa mataifa hupokea maombi zaidi ya elfu 3 kutoka sehemu mbalimbali na kisha kufanya mchanganua na kupitisha maombi yanayokidhi vigezo.