Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO kuzindua ramani ya matatizo ya kuumwa kichwa

WHO kuzindua ramani ya matatizo ya kuumwa kichwa

Ripoti ya shirika la afya duniani WHO inasema kuwa watu wengi zaidi wanakabiliwa na matatizo ya kuumwa na kichwa.

Ripoti hiyo inasema kuwa nusu ya robo tatu ya watu walio kati ya umri wa miaka 18 na 65 kote duniani waliumwa na kichwa mwaka uliopita. Inaongeza kuwa ni watu wachache walio na matatizo ya kuumwa na kichwa kote duniani wanaofanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Kote duniani karibu asilimia 50 ya watu walio na matatizo ya kichwa huwa wanajitibu wao wenyewe bila ya kuwatembelea madakatari.