Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwajibikaji unahitajia kuokoa maisha ya mama na mtoto

Uwajibikaji unahitajia kuokoa maisha ya mama na mtoto

Tume iliyobuniwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuchunguza usaidizi unaotolewa katika kuokoa maisha kwenye nchi zinazoendelea imetoa mapendekezo yake mapya.

Mapendekezo hayo yalitangazwa mjini Dar es Salaam nchini Tanzania na tume ya Umoja wa Mataifa inayohusika na habari na uwajibikaji katika masuala ya kiafya kwa akina mama na watoto. Tume hiyo inaongozwa na rais wa Tanzania Jakaya kikwete kwa ushirikiano na waziri mkuu wa Canada Stephen Harper.

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro alihudhuria warsha hiyo na anaeleza wajibu wa tume hiyo.

(SAUTI YA ASHA ROSE MIGIRO)