Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNFPA kuzindua ripoti ya kwanza kabisa kuhusu ukunga

UNFPA kuzindua ripoti ya kwanza kabisa kuhusu ukunga

Shirika la Umoja la Mataifa la kutetea maslahi ya watu UNFPA linatarajiwa kuzindua ripoti ya kwanza kabisa kuhusu ukunga mwezi Juni mwaka huu.

UNFPA masema kuwa mwanamke mmoja kati ya wanawake watatu kwenye nchi zinazoendelea anajifungua yeye mwenyewe au kwa usaidizi wa watu wa familia.

Inakadiriwa kuwa wanawake 1000 uaga dunia huku pia watoto 5,500 wakifa kila wiki ya kwanza ya kuzaliwa kutokana na kutokwepo kwa huduma bora. UNFPA pia inakadiria kuwa kuna uhaba wa wakunga waliohitimu 350,000 kote duniani.