Skip to main content

Banaitaka dunia kutokomeza silaha za maangamizi

Banaitaka dunia kutokomeza silaha za maangamizi

Nchi zote duniani zimetolewa wito na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kufanya kila liwezekanalo kutokomeza silaha za maangamizi.

Ban ametoa wito huo katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kuwakumbuka waliopoteza maisha kutokana na vita vya silaha za maangamizi. Siku hii pia inaadhimisha kumbukumbu ya kuanza kwa utekelezaji wa mkataba wa kimataifa kupinga silaha za maangamizi uliopitishwa April 29 mwaka 1997.

Ban amesema siku hii ni fursa ya kuwakumbuka wahanga wa silaha hizo na kurejea msimamo wake kwa jumuiya ya kimataifa kulaani matumizi ya kile alichokiita unyama wa silaha za maangamizi. Amesema hatua zimepigwa kuondoa tishio kukomesha silaha hizi huku asilimia 90 ya mitambo ya uzalishaji wa silaha hizo haifanyi kazi au imegeuza kuwa na matumizi ya amani.