Saudi Arabia yasaidia ukarabati wa makazi ya wakimbizi Gaza: UNRWA

Saudi Arabia yasaidia ukarabati wa makazi ya wakimbizi Gaza: UNRWA

 Zaidi ya familia 7,000 ya wakimbizi walioko katika ukingo waGazawatapatiwa msaada wa fedha ili kuzifanyia ukarabati nyumba zao zilizoharibiwa wakati wa mashambulizi ya mwezi Novemba mwaka jana. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhududumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limepokea kiasi cha dola za marekani milioni 15.6 kutoka kwa mfuko wa Maendeleo wa Saudia Arabia ili kufanikusha ujenzi wa makazi hayo. Robert Turner, ambaye ni Mkurugenzi wa INRWA amesema kiasi hicho cha fedha kimetolewa wakati muafaka ikiwa ni miezi minne tangu kufanyika mashamabulizi hayo ambayo pia yalisabisha vifo vya raia kadhaa. Ameeleza kuwa, kwa kipindi kirefu shirikahilohalijapata kuendesha zoezi la ukarabati katika maeneo yaliyokumbwa na mashambulizi lakini sasa zoezi hili linafanyika katika muda mfupi. Ameshukuru mfuko wa maendeleo wa Saudia akisema kuwa imeonyesha moyo wa ukarimu.