Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwekezaji wa nje umeongezeka:UNCTAD

Uwekezaji wa nje umeongezeka:UNCTAD

Taarifa iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la biashara, uchumi na maendeleo UNCTAD inaonyesha kwamba uwekezaji wa moja kwa moja wa nje umeongezeka kwa asilimia 13 kwa mwaka 2010 ingawa uko chini kidogo ya ule wa 2007 kabla ya mdororo wa uchumi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya UNCTAD kuongezeka huko kumetokana na uwekezaji ulioanzia nchi zinazoendelea na nchi za uchumi ulioko kwenye kipindi cha mpito ambazo zimechangia asilimia 30 ikilinganishwa na 15 ya mwaka 2007.

Hata hivyo UNCTAD inasema kwa Afrika uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje umepungua zaidi 2010 na kufikia dola bilioni 4 ikilinganishwa na dola bilioni 4.5 za 2009. Libya na Afrika Kusini nchi mbili zinazowekeza moja kwa moja nje uwekezaji wake umepungua sana Astrit Sulstarova ni afisa wa masuala ya uchumi wa UNCTAD.

(SAUTI YA ARSTRIT SULSTAROVA)