Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya kimataifa ya kuenzi wanazuoni

Leo ni siku ya kimataifa ya kuenzi wanazuoni

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kuenzi wanazuoni mwaka huu inajikita katika jukumu la ubunifu kwenye masoko, katika jamii na muundo wa ubunifu wa siku za usoni.

Siku hiyo ambayo huadhimishwa kila mwaka April 26 kauli mbiu ya mwaka huu ni ubunifu wa siku zijazo. Akizungumzia jukumu la ubunifu mkurugenzi wa shirika la kimataifa la wanazuoni WIPO, bwana Francis Gurry amefafanua ubunifu kama ni lugha ya mawasiliano ya vitu, na ukweli ni kwamba misingi yake inatofautisha vitu mbalimbali vinavyotengenezwa kuanzia bidhaa za nyumbani kama viti na meza hadi vifaa vinavyotumia teknolojia ya hali ya juu.

Katika siku hii WIPO inachagiza wabunifu kutengeneza bidha zinazovutia, rahisi kutumia na zenye usalama kwa kusaidia kulinda uhalisi wa bidhaa hizo kutokana na hatari ya kughushi na kuigizwa na watu wengine.