Ban ataka hatua zaidi kuchukuliwa kuzuia vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Malaria
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa lengo la kumaliza kabisa vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa Malaria ifikapo mwaka 2015 linaweza tu kutimizwa ikiwa jitihada zaidi zitachukuliwa katika vita dhidi ya ugonjwa huo.