Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utandawazi ni kitovu cha maendeleo yasema:UNCTAD

Utandawazi ni kitovu cha maendeleo yasema:UNCTAD

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa katika kitengo kinachohusika na biashara na maendeleo UNCTAD zimesema kuwa kwenye mkutano ujao agenda kuu iliyopendekezwa ni ile inayozangatia utandawazi wenye tija ya maendeleo kwa wote.

Mkutano huo ambao utafanyika huko Doha, Qatar  kuanzia April 26 hadi 26 mwaka ujao wa 2012 ni wa 13 ambao pia anatazamia kuzingatia eneo la uwezeshaji wa maendeleo endelevu.

Mkutano wa mwisho kama huo ulifanyika mwaka 2008 nchini Ghana. Mkutano huo ni jukwaa huru linalotoa fursa kwa nchi wanachama kujadilia mwelekeo halisi wa uchumi wa dunia na namna ya kuzikabili changamoto za kiuchumi.