Skip to main content

WFP kutumia teknolojia kuchangisha fedha za chakula

WFP kutumia teknolojia kuchangisha fedha za chakula

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limezindua mpango mpya ambapo linatumia vyombo vya habari vinavyohusika na masuala ya kijamii kuchangisha fedha zinazohitajika kuwalisha maelfu ya watoto walio na njaa kote duniani.

Mpango huo ujulikano kama WeFeedback unawawesesha wanaouunga mkono kueleza ni watoto wangapi wanaweza kuwalisha kwa kutoa fedha za bei ya chakula fulani kinachopendwa na watoto. Kupitia mpango huo wafuasi wake pia wanaweza kufuatilia na kufahamu idadi ya watoto wanaolishwa na jamii zao na ni chakula cha aina gani kinachotolewa sehemu mbali mbali za dunia.

Emilia Casella ni msemaji wa WFP.

(SAUTI YA EMILIA CASELLA)